Medical OPD Clinic

Posted on: September 18th, 2024

TAARIFA FUPI JUU YA KLINIK YA MOYO NA SUKARI:

  • Katika hospitali ya Mkoa wa Tabora –KITETE kuna aina mbalimbali za klinik zinazofanyika miongoni mwa kliniki hizo ni pamoja na kliniki ya moyo pamoja na sukari.
  • Kliniki ya moyo hufanyika kila siku ya jumanne ya kila wiki ambapo wagonjwa wote wenye matatizo ya moyo huonwa na daktari maalum katika kliniki hiyo.
  • Kliniki ya Ugongwa wa kisukari hufanyika kila siku ya alhamisi ya kila wiki ,ambapo pia Daktari maalum hukaa na kuwaona wagonjwa hao.
  • Kliniki hii inafanya kazi kwa wiki mara mbili kama ilivyoainishwa hapo huu isipokua siku za mapumziko maalum ya kiserikali.
  • Kliniki hii inaona wagonjwa wa aina zote ,Wagonjwa wanaotumia bima,wagongwa wanaolipia huduma papo kwa papo na pia wale ambao hutibiwa kwa msamaha kwa mujibu wa sheria.
  • Katika kliniki yetu wagonjwa wote ni sawa,fika upate huduma iliyo bora
  • Imeandaliwa na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya ndani

                                                                   Dkt.Nassoro I. Kaponta.